.
26th November, 2016
Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen ametaka baadhi ya wanachama wa kamati ya bunge kuhusu uhasibu kuchunguzwa, akidai kuwa wanahujumu uchunguzi unaofanywa kuhusu wajibu wa aliyekuwa waziri wa ugatuzi Anne Waiguru katika fedha za nys zilizopotea. Murkomen amemlaumu mbunge wa Suba John Mbadi akidai kuwa ameingiza siasa katika suala hilo. Murkomen alitajwa na Bi Waiguru kuwa miongoni mwa waliofaidi katika sakata hiyo