.
29th October, 2016
Sakata ya shilingi bilioni tano katika Wizara ya Afya inazidi kuibua masuali mengi ya kisiasa. Seneta wa Machakos Johnstone Muthama amependekeza kuwe na maandamano katika hatua ya kukashifu ufisadi nchini. Hata hivyo kampuni inayohusishwa na dadake rais Uhuru Kenyatta imekanusha kushiriki katika ufisadi huo na kusema siasa zimeingizwa katika suala hilo.