.
12th October, 2016
Bunge la Afrika mashariki bado linajadili hoja ya kushinikiza baraza la mawaziri kufanya kikao cha dharura ili kutatua suala la uhaba wa fedha. Shughuli zote zimelemazwa kwa zaidi ya mwezi mmoja wakati baraza hilo na marais wanachama walitia saini bajeti ya mwaka huu lakini hadi sasa wamesalia kutegemea misaada kutoka jamii ya kimataifa. Mwanahabari Francis Mtalaki ambaye yuko Zanzibar panapofanyika vikao alizungumza na mdhamini wa hoja hiyo Judith Pareno na kutuandalia taarifa ifuatayo.