3rd October, 2016
Waumini wa dhehebu la akorino maeneo ya Embu wamelalamikia kutengwa na serikali ya Kenya. Waumini hao waliokusanyika katika shule ya upili ya Kangaru kaunti ya Embu wamesema wana wasiwasi kuhusu kuhusishwa kwao kwenye vyeo serikalini na pia wanafunzi wa dini kuruhusiwa kuvaa vilemba shuleni kama dini zingine.