Mvuvi wa miaka 39 aaga dunia baharini huko Malindi
12th September, 2016
Mvuvi mmoja wa umri wa miaka 39 amekufa maji katika bahari ya Hindi karibu na eneo la Mayungu –Malindi. Bidii Katana Shombo aliyejulikana kama mpiga mbizi hodari aliamkia uvuvi mapema lakini ukageuka kuwa mkosi.