12th September, 2016
Maelfu ya waumini wa dini ya kiislamu leo wamekongamana katika misikiti na viwanja mbalimbali kwa sala ya kuadhimisha sikukuu ya Idd-ul-Adha sikukuu hii hufahamika zaidi kama idd ya kuchinja ambapo waumini hukumbuka jinsi Abrahamu alivyowekwa kwenye majaribu ya kumtii mungu kwa vyovyote. Alitakiwa kumtoa mwanawe wa kiume kama sadaka lakini mungu akampa kondoo alipoonesha nia ya kumtii. Katika kaunti ya Isiolo, viongozi wa dini waliwarai waumini waliohudhuria sala hiyo katika uwanja wa kaunti ya Isiolo kudumisha amani. Kule Mombasa sala ya kuadhimisha sikukuu ya Idd ilifanyika katika shule ya msingi ya Ronald Ngala. Viongozi waliohudhuria hafla hiyo wamesisitizia umuhimu wa amani na utangamano nchini. Isitoshe wamekashifu shambulizi la jana ambapo kituo cha polisi kilivamiwa na kundi la wanawake waliokuwa na bomu la petroli na silaha nyengine.