7th September, 2016
Mtazamaji je, ushawahi kuyanywa maziwa ya punda maishani mwako? Wafugaji sasa wamegundua kwamba maziwa ya punda ni matamu na salama kwa matumizi ya binadamu. Hiyo ni faida moja tu ya mfugo punda mbali na kuhalalaishwa kwa nyama yake tangu mwaka wa 2014 humu nchini. Mwanahabari wetu Lofty Matambo alikutana na mfugaji John Nduhiu katika kaunti ya Naivasha anayemsifu punda kwa maziwa yake na kumsomeshea watoto mbali na kumjengea nyumba, lakini iwapo utawapoteza punda wako 17 wanaokufaidi kwa usiku mmoja utachukua hatua gani? Ndo simulizi za wafugaji punda wengi wakilaani uwepo wa kichinjio cha punda cha Goldex kilichoko kaunti ya Baringo. Undani uko hapa katika makala ya nifae nikufae .