Wanaokimezea mate kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa wanazidi kuongezeka
6th August, 2016
Wanaokimezea mate kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa wanazidi kuongezeka. Anania Mwaboza mshauri wa naibu rais amejitosa rasmi na kuondoa uvumi wa iwapo alisalimu amri. Mwaboza atalazimika kumenyanya na Suleiman Shabal kuwania tiketi ya chama cha Jubilee iwapo URP na TNA zitawekwa kwenye kikapu kimoja. Je, kulikoni Mombasa? Francis Mtalaki ametuandalia taarifa hiyo kwa kina