Matamshi ya Raila yakosolewa baada ya ziara yake magharibi
26th July, 2016
Ziara ya siku tano ya kiongozi wa odm Raila Odinga sehemu ya magharibi, ilichukuliwa na wengi kama iliyonuia kuzima uasi uliochipuka ndani ya chama. Lakini siku kadhaa baada ya ziara hiyo, yamkini sauti hizo bado zinasikika, huku viongozi wengine ndani ya muungano wa cord wakionekana kupanda basi lake aliyekuwa katibu mkuu wa ODM na mbunge wa Budalang’i Ababu Namwamba. Je, ziara ya Raila Odinga ilifaulu au ilizaa uasi zaidi katika eneo hilo?. Mwandishi wetu wa magharibi Robert Wanyonyi anatathmini swala hilo.