Bi. Linah Jebii Kilimo awaonya vikali wahudumu wa afya Kisii kwa kukithiri kwa ukeketaji
17th December, 2015
Juhudi za kupiga vita tohara kwa mtoto wa kike katika jamii ya Wakisii inakumbwa na changamoto chungu nzima. Inadaiwa kuwa baadhi ya wahudumu wa afya wamekuwa wakiwapasha tohara wasichana kisiri. Mwenyekiti wa bodi ya kushughulikia maswala ya ukeketaji Bi. Linah Jebii Kilimo aliwaonya vikali wahudumu wa afya.