Mama amkana binti akidai akosa maadili kule Mariakani, Kilifi
18th May, 2015
Je mtoto wako akikushinda kulea kwa madai kuwa anakutusi au mnapigana, utafanyeje? Ndilo swali ambalo limejiri kule mariakani kilifi ambapo mama mmoja amemkana bintiye na kumfukuza nyumbani licha ya msichana huyo kudaiwa kuwa na tatizo la afya. Msichana huyo sasa ameokolewa na jirani ambaye sasa anataka serikali kuingilia kati na kumsaidia msichana huyo. Je ni ulezi umeenda kombo au kulikoni?