Ibada ya wafu ya Fidel Odinga yafanyika All Saints Cathedral
8th January, 2015
Misa ya wafu kwa mwendazake, Fidel Odinga imefanywa hii leo katika kanisa la All Saints Cathedral hapa Nairobi. Ibada hiyo ilihudhuriwa na wakenya wa tabaka mbali mbali huku rais uhuru kenyatta, akiandamana na naibu wake William Ruto , magavana, maseneta, na wabunge . Jamaa na marafiki walimtaja Fidel Odinga kuwa mtu aliyewapenda watu na ambaye hakuathirika kwa mipaka ya tabaka au jamii. Rais uhuru kenyatta alitumia fursa hiyo kuwaomba wakenya kudumisha umoja.