Watu wawili wafariki na wengine wane kujeruhiwa vibaya Turkana
16th March, 2014
Watu wawili wamefariki na wengine 4 kujeruhiwa vibaya katika kijiji cha kakongu kaunti ya turkana.
Mauaji haya yametekelezwa na wavamizi usiku wa kuamkia leo. Majeruhi wanapokea matibabu katika hospitali ya wilaya ya Lodwar. Inadaiwa kundi la wavamizi wapatao mia tano mwendo wa saa nne usiku walikivamia kijiji hicho na kufyatua risasi kiholela na kumuua mtu mmoja. Wakaazi waliokuwa na ghadhabu waliandamana na kutatiza shughuli za usafiri kwa kuziba barabara ya kutoka Lodwar kuelekea kitale. Maafisa wa gsu walilazimika kuingilia kati na katika makabiliano na wananchi mmoja wa waandamanaji alipigwa risasi na kufariki. Yadaiwa wavamizi hao walitoweka na mifugo elfu mbili.