Mahakama yaamuru Mutea Iringo kukamatwa kwa kukosa kufika mahakamani
24th February, 2014
Mahakama kuu imetuma ombi kwa inspekta mkuu wa polisi David Kimaiyo la kukamatwa kwa katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani Mutea Iringo. Agizo la kukamatwa kwa iringo limetolewa tena baada ya iringo kukosa kufika mahakamani mnamo tarehe 11 februari bila kutoa sababu yoyote. Mutea anapaswa kufika mahakamani ili kutoa maelezo kuhusu kukosa kuheshimu uamuzi wa mahakama kuhusu raia mmoja wa tanzania aliyefungwa nchini kwa madai ya wizi wa kimabavu. Alfred koroso alifungwa mwaka wa 1993 na baadaye ikatambulika kuwa hakuwa na hatia. .ingawa mwaka wa 2008 mahakama iliamuru serikali kumpa koroso shilingi milioni 21 kufikia sasa mwathiriwa hajapewa fidia hiyo. Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 12 mwezi machi.