Mahojiano: Ana kwa Ana na mwanaharakati Boniface Mwangi
16th February, 2014
Pale jina boniface mwangi linapotajwa, kinachokujia akilini mwako mtazamaji ni mwanaharakati anayeendeleza maandamano dhidi ya serikali, huku picha za kupigwa na maafisa wa polisi na kurushiwa vitoza machozi zikiwa si geni. Ni kijana aliyebadilisha sura ya maandamano humu nchini kwa kutumia talanta yake ya kisanii kama vile kutumia nguruwe kuashiria ulafi wa wabunge, kuunda vikaragosi aina ya watoto wachanga akiashiria japo kenya ina miaka hamsini, bado viongozi wake hawajakomaa kuleta maendeleo. Lakini je, ni kwanini akaamua kusita kuendelea na maandamano kama haya, japo wengi wanamtarajia kuendelea na vuta nikuvute kati yake na maafisa wa polisi.