Dereva wa ajali ya Mtindwa afikishwa Kortini na kufunguliwa mashtaka ya mauaji
31st October, 2013
Dereva wa matatu iliyohusika jana kwenye ajali mbaya na gari la moshi eneo la mutindwa na kusababisha vifo vya watu 12 amefikishwa leo kizimbani akikabiliwa na mashtaka ya mauaji ya watu 9. Wakati huo huo, chama cha maslahi ya wenye matatu kimewataka wenye magari ya abiria pamoja na vyama vya ushirika vya magari ya usafiri kuwafuta madereva wenye kiburi na wasio na maadili mema kama hatua moja ya kupunguza ajali barabarani.