Henry Kosgey apata upinzani kutoka mwanawe Alex
23rd February, 2013
Wadhifa wa Useneta kaunti ya Nandi, ndio unatazamiwa kuibua msisimko si haba. Mbali na mapambano kati ya chama cha ODM na URP….kinyanganyiro kimetiwa ladha na mapambano kati ya baba na mwanawe. Herny Kosgey aliyetawala siasa za Nandi kwa miongo mitatu anawania kiti kwa tiketi ya chama cha ODM, mpinzani wake ni Stephen Sang wa URP ambaye anaungwa mkono na mwanawe Kosgey Alex Kigen Sang. Alex anawania ubunge wa Emgwen kwa tiketi ya URP….je Machi nne ni Kosgey yupi atampiku mwenzake?