.
27th January, 2022
Mashabiki wa soka nchini wanaendelea kuomboleza kifo cha shabiki mwenzao mashuhuri Isaac Juma ambaye anakumbukwa na wengi kwa kuhudhuria mechi za soka za timu ya taifa Harambee Stars akiwa amejipaka rangi za kila aina mwilini akicheza uwanjani na bendera ya taifa.
Isaac Juma aliuawa kwa kukatwakatwa na upanga na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake huko Mumias katika kile kinasemekana kuwa ni mzozo wa umiliki wa ardhi.