25th January, 2022
Ni afueni kwa jaji wa mahakama ya Rufaa Sankale Ole Kantai baada ya mahakama kuu kuagiza tume ya huduma za mahakama nchini, JSC, kutoendelea na kesi dhidi Ya Jaji Sankale.
Tume hiyo ilikuwa imepokea maombi mawili ya kumchunguza Jaji Sankale na kupendekeza kutolewa ofisini. Akitoa agizo hilo, Hakimu Anthony Mrima alisema maombi hayo mawili yawekwe pamoja na kusikizwa kama ombi moja.