25th January, 2022
Chama cha UDA kinachomwegemea Naibu Rais William Ruto leo kimetangaza bodi ya uchaguzi itakayosimamia kura ya mchujo ya chama hicho kuwateua wawaniaji wa nyadhfa zote za uongozi chamani.
Naibu wa Rais William Ruto alizindua bodi hiyo rasmi saa chache baada ya kufanya kikao na viongozi kutoka laikipia alipotetea muungano wake wa hivi juzi na kinara wa ANC Musalia Mudavadi.