27th December, 2021
Wakazi wa eneo la Mogotio kaunti ya Baringo waliamkia kisa cha kuatua moyo baada ya mshukiwa mmoja wa mauaji ambaye alikuwa chini ya mbawa za polisi kuwaelekeza polisi kufukua makaburi ya mkewe na mawanawe anayesemekana kuwaua na kuwazika. Mshukiwa Moses Kipchirchir Ruto anadaiwa kuwaua watu watatu kwenye mazingira tata.