16th December, 2021
Siku chache baada ya chama kipya cha democratic action party of kenya, SAP-K, kuzinduliwa nyufa zinaonekana kuanza kuibuka mapema baada ya aliyekuwa waziri na mbunge wa kwanza noah wekesa kuibuka na lalama kuwa alipokonywa nafasi yake ya kuwa mwenyekiti wa chama hicho kipya. wekesa sasa anautaka uongozi wa chama hicho kumwomba msamaha kwa kuvunja ahadi ya kwamba angekuwa mwenyekiti na kisha wadhafa huo kipewa mbunge wa kanduyi wafula wamunyinyi.