3rd December, 2021
Seneta wa Baringo Gideon moi, amewataka viongozi wote wa kisiasa pasi na kuzingatia mirengo, kujitokeza ili kutafuta suluhu la kudumu la matatiizo yao ya ardhi. Moi aliyekuwa akizungumza katika eneo la sagamion huko Narok Kusini kaunti ya Narok amesema kuwa inasikitisha kuwa kuna hali duni miongoni mwa watu waliomiliki ardhi katika msitu wa mau, baada yao kufurushwa bila kupewa sehemu mbadala.