2nd December, 2021
Wachimba migodi wanane wamekwama ndani ya migodi miwili ya dhahabu iliyoporomoka katika kijiji cha Abimbo eneo la Bondo kaunti ya Siaya.
Kwa mujibu wa OCPD wa eneo hilo Rosyline Cheboso wachimba migodi wawili wameokolewa na juhudi zinaendelea kuwaokoa wachimba migodi wanane waliokwama ndani ya migodi hiyo.
Odeo Sirari amezungumza naye kwa njia ya simu muda mfupi uliopita.