2nd December, 2021
Kiongozi wa chama cha ANC, Musalia Mudavadi amekosoa matamshi ya Rais Uhuru Kenyatta hapo jana, ambapo alionekana kumpigia debe kinara wa Odm Raila Odinga kuwa mrithi wake baada ya uchaguzi mkuu ujao.
Mudavadi, ameonekana kumtetea Naibu Rais William Ruto, akisema hakuna mtu aliye na mamlaka ya kuwaamulia wakenya kuhusu ni nani anayefaa kuwaongoza.