30th November, 2021
Mkutano wa jopo la pamoja la ushauri kuhusu matayarisho ya uchaguzi mkuu ujao uliopaswa kufanyika watibuka. Hii ni baada ya tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kujiondoa kama mdao mkuu kwenye jopo hilo na kusababisha Jaji Mkuu Martha Koome, Waziri wa Usalama Fred Matiang'i na Joe Mucheru wa mawasiliano kuahirisha kwa muda mkutano huo na kuuwacha kwenye njia panda hatma ya jopo hilo.