25th October, 2021
Jeshi nchini Sudan limevunja serikali ya Kiraia na kuwakamata viongozi wa kisiasa na kisha kutangaza hali ya hatari nchini humo. Jenerali Abdel Fattah Burhan, ambaye amekuwa akiongoza baraza la pamoja na viongozi wa kiraia amesema kumekuwa na migogoro mingi ya kisiasa nchini humo.