.
25th October, 2021
Seneta wa Lamu Anwar Oleitiptip ameaachiliwa huru kwa dhamana na mahakama ya nanyuki baada ya kujisalimisha jumapili jioni kuhusiana na tukio ambapo mwanamke mmoja alijeruhiwa kwa kupigwa risasi katika eneo la Nanyuki. Seneta huyo anatuhumiwa kwa kumpiga risasi mwanamke huyo baada ya ugomvi kuzuka baina yao usiku wa kuamkia jumapili. Ombi la polisi la kutaka kuendelea kumzuilia mshukiwa lilitupiliwa mbali na hakimu mkaazi Vincent Masivo akisema kuwa sababu zilizotolewa na upande wa mashtaka hazina uzito.