20th October, 2021
Upasuaji wa mwili wa Masten Wanjala aliyeuawa na umati huko Bungoma unaonyesha kuwa mshukiwa huyo wa mauaji ya watoto kumi na watatu alifariki kutoka na majereha yaliyosababishwa na vifaa butu. Masten alishambuliwa na kuuawa na umati uliojawa na hasira katika kijiji cha Mukhweya baada ya yeye kutoroka korokoroni jijini Nairobi pale ambapo alikuwa anatarajiwa kufunguliwa mashtaka ya mauaji. Mwili wa mshukiwa huyo ulifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Bungoma na wanapathologia waserikali. Masten sasa anatarajiwa kuzikwa katika kijiji cha Mukhweya.