.
13th October, 2021
Eneo la magharibi hususan kaunti ya Kakamega inajulikana sana kutokana na mashindano ya vita vya fahali ila pia mashindano ya vita vya jogoo yana umaarufu wake. Shindano la vita vya jogoo limekuwa maarufu na kuwavutia maelefu ya mashabiki kwa miaka na mikaka katika eneo hilo. Mwanahabari wetu Willy Lusige alikutana na mmoja wa wakufunzi wa jogoo wanaoshiriki mashindano hayo ambaye anadai ana uwezo wa kuzungumza na kuku hao wakati wa mafunzo.