13th October, 2021
Kiongozi wa ODM Raila Odinga, leo ameendeleza kampeni zake hapa jijini nairobi, huku akieleza kuhusu ajenda yake ya kugawa shilingi elfu sita kwa kila familia ya walalahoi, endapo atachaguliwa kuwa Rais. Raila pia alitumia fursa hiyo kuwarai vijana kujitokeza na kujiandikisha kuwa wapiga kura.