.
20th September, 2021
Wanasiasa kutoka eneo la Mlima Kenya wamekutana kwa mara nyingine tena katika eneo la Naivasha kupanga mikakati kuelekea katika uchaguzi mkuu ujao. Viongozi hao akiwemo kiongozi wa chama cha Narc Kenya wanasema sasa wamepata muafaka wa kisiasa na watazungumza kwa sauti moja kutafuta ushirikiano na viongozi kutoka maeneo mengine.