.
20th September, 2021
Tume ya kitaifa ya Uiano na maridhiano NCIC inampango wa kuzindua muongozo unaopania kuwatwika jukumu la kudumisha amani wanasiasa kabla na wakati wauchaguzi. Kulingana na mwenyekiti wa tume hiyo Samuel Kobia muongozo huo utawalazimu wanasiasa kuwa waangalifu wanapoendeleza kampeni zao kuelekea uchaguzi mkuu ujao.