16th September, 2021
Kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi ameitaka serikali kufanyia marekebisho mfumo wa matozo ya ushuru kwa bidhaa za petroli kwa vile mfumo wa sasa umepelekea gharama ya maisha kupanda na kuhangaisha wananchi kutokana na mfumuko wa bei. Idhini ya wabunge kuiruhusu serikali kuweka ushuru wa V.A.T kwa bidhaa za petroli mwaka 2018 ndio chanzo cha mfumuko wa bei ya mafuta.