3rd August, 2021
Maafisa wa itifaki katika afisi ya Rais wamelaumiwa kutokana na kisa kilichoshuhudia katika uwanja wa ndege wa Wilson hapo jana ambapo Naibu Rais William Ruto alizuiwa kusafiri nchini Uganda. Akiwasilisha hoja bungeni mbunge wa Ruaraka Tom Kajwang’ alisema kizaazaa hicho kilimshushia hadhi Naib Rais na pia kuzua shauku kuhusu safari hiyo na sasa ni lazima maafisa wa itifaki waelezee bayana ni yapi yanayotokota. Hata hivyo wabunge wanamuunga mkono Ruto walimzomea kajwang wakidai alikuwa akiwakejeli.