2nd August, 2021
Palishuhudiwa kizaazaa katika taasisi ya mafunzo ya kibiashara ya bahati huko nakuru, baada ya wanafunzi wenye hamaki kuzua rabsha wakitaka kuelezwa ni kwa nini hawajapewa mtihani, licha ya wao kulipa karo yote na kuhudhuria masomo yao ifaavyo. Kulingana na wanafunzi hao, ubadhirifu wa fedha na usimamizi mbaya wa taasisi hiyo ndicho chanzo kikuu. Lakini kama anavyoarifu ibrahim karanja, usimamizi wa taasisi hiyo umesema kuwa wanafunzi hao hawako tayari kuufanya mtihani unaosimamiwa na baraza la mitihani nchini knec, kwa kuwa hawajatekeleza matakwa yote.