2nd August, 2021
Mbunge wa Kimilili Didmus Barasa alifikishwa mbele ya mahakama ya Bungoma na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki moja baada ya video kusambaa ikionyesha akimzaba kofi mwanamme mmoja aliyetajwa kama mwanakandarasi wa ujenzi wa madarasa aliyefunga milango ya madarasa katika shule moja eneo bunge lake akidai malipo ya kazi aliyoifanya.