1st August, 2021
Shirikisho la soka nchini FKF limeziadhibu Gor Mahia na AFC Leopards kwa kukosa kufika uwanjani thika kushiriki debi la mashemeji. Kwa mujibu wa fkf hatua ya timu zote mbili zilisababisha hasara kwa wadhamini wa ligi na vyombo husika vya matangazo. Wenyekiti wa Gor Mahia na AFC Leopards wamepigwa marufuku ya muda kushiriki shughuli zote za kandanda. Mbali na marufuku hiyo timu zote zimenyanganywa alama tatu na kupigwa faini ya milioni kumi kwa ujumla.