16th June, 2021
Mzozo kuhusiana na umiliki wa kipande cha ardhi katika kisiwa cha Wasini kaunti ya Kwale unaendelea na kuna hofu kuwa makubaliano yasipoafikiwa kwa haraka huenda ukazua janga kubwa. Kwa upande mmoja mahakama imeiruhusu familia moja kuchukua ekari 289 zinazozozaniwa ilhali upande mwengine wenyeji wanadai kuwa ni chache ya ekari hizi tu ambazo familia hii inafaa kumiliki. Juhudi zozote za kupima ardhi hiyo zimezuiwa na wenyeji ambao wameapa kutowaruhusu maafisa wa ardhi Kisiwani.