16th June, 2021
Karim Khan ambaye alikuwa wakili kwenye mashtaka dhidi ya Naibu Rais William Ruto katika mahakama ya ICC ameapishwa kama mwendeshaji mashtaka kwenye mahakama hio mapema hii leo. Khan anachukuwa nafasi ya aliyekuwa mwendeshaji mashtaka Fatou Bensouda akitarajiwa kuendesha mashtaka kwenye mahakama hio ikiwemo mashtaka ya makosa ya jinai katika maeneo mbali mbali ulimwenguni.