.
16th June, 2021
Huku uhasama na tofauti kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto ukiendelea kutokota, Ruto sasa anaonekana kuchukua mkondo tofauti wa kumjibu hadharani Rais katika vita vyao. Kwa siku za hivi karibuni, Ruto amekuwa akitumia mitandao ya kijamii kutoa kauli zake dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta kinyume na jinsi amekuwa akinyenyekea katika mikutano ya hadhara.