.
9th June, 2021
Serikali imezindua sera mpya itakoyoongoza elimu ya mazoezi ya viungo vya mwili na michezo kwa mujibu wa kanuni za utekelezaji wa mtaala wa CBC. Waziri wa elimu, Profesa George Magoha, amesema lengo ni kugeuza michezo na kuifanya kuwa taaluma inayofunzwa kwa kuzingatia mwelekeo na vigezo vya mtaala, sawa na yalivyo masomo mengine.