x News The Standard Digital KTN Prime KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS Tutorsoma Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
x
x

Dimba la Betway: Bandari FC waizaba Dimba Patriots kutoka Nairobi mabao 5-1

02, Jun 2021

Mabingwa watetezi wa kombe la FKF Bandari wametoa onyo kwa wapinzani wenza baada ya kuzaba Dimba Patriots kutoka Nairobi mabao 5?1 katika mchuano ulioandaliwa mbaraki na kujikatia tiketi ya raundi ya 16 bora. Benjamin Misha alicheka na wavu mara mbili katika mchuano huo. Bandari walitwaa taji hili mwaka wa 2019 baada ya kulaza Kariobangi Sharks katika fainali japo virusi vya korona vikasitisha uetezi wao mwaka jana. washindi wa dimba hili hushiriki katika michuano ya barani hivyo basi hawakuwa na huruma dhidi ya Dimba Patriots walio katika daraja la nne katika ligi ya FKF. Benjamin Mosha alifungua ukurasa wa mabao dakika ya 18 kupitia nipe nikupe zake na mganda William Wardi. Wardi aliongeza la pili baada ya muda wa maoumziko dakika ya 66. Wageni walipunguza aibu dakika ya 68 kupitia kwa Rashid Athman. Darius Msagha aliongezea bandari la tatu dakika ya 73, mosha akapachika lake la pili, kisha yema mwana akahitimisha kichapo kwa la tano.

RELATED VIDEOS


Feedback