.
1st June, 2021
Uhasama kati ya nguzo ya utawala wa Rais na idara ya mahakama kwa mara nyingine tena umejitokeza katika sherehe za siku kuu ya madaraka mjini Kisumu huku Rais Uhuru Kenyatta akiishtumu mahakama kwa kile anachosema kuwa ni kuhujumu nia ya wakenya katika uamuzi wa mahakama kuu kuharamisha mchakato wa marekebisho ya katiba kupitia mswada wa BBI. Kadhalika tofauti kati ya Rais na Naibu wake ikajitokeza tena, Naibu Rais William Ruto akisisitiza umuhimu wa kuheshimu taasisi za utawala kinyume na semi za Rais akitaka mahakama kuwajibikia maamuzi yake ambayo anasema yamelisababishia taifa hasara ya zaidi ya shilingi trillioni moja.