26th May, 2021
Kijana mmoja kutoka kaunti ya Isiolo ambaye aliwahi kugombea kiti cha MCA cha bulapesa na kutofanikiwa mwaka 2017, ameibuka wa kwanza kujitosa kwenye kilimo cha samaki katika kaunti ya isiolo. Robert mugambi mwenye umri wa miaka 35 anasema amenufaika pakubwa na kilimo hicho licha ya changamoto ambazo amekumbana nazo. mugambi anasema alipata wazo hilo baada ya kufilisika alipotumia fedha zake zote kufanya kampeni kwenye uchaguzi mkuu uliopita.