15th May, 2021
Timu ya Afc Leopards imeimarisha matumaini yake kutwaa taji la ligi kuu msimu huu kufuatia ushindi wake wa goli moja bila jibu dhidi ya Nzoia Sugar. Kwengineko, licha ya kucheza wachezaji kumi pekee, timu ya KCB imelazimisha sare tasa dhidi ya viongozi Tusker huku Bidco united ikiikamua sare Bandari ugani mbaraki. Western Stima nayo imeandikisha sare ya goli moja dhidi ya Posta Rangers.