.
15th May, 2021
Timu ya taifa ya raga ya wachezaji saba kila upande Shujaa imemaliza katika nafasi ya pili kwenye shindano la solidarity ambalo limekamilika hii leo Afrika Kusini. Shujaa ilianza kwa kuinyuka uganda alama 31 kwa 7 kabla ya kuadhibiwa na wenyeji afrika kusini alama 31 kwa 5 katika fainali. Mchuano huo umetumika kama maandalizi ya mashindano ya olimpiki.