.
15th May, 2021
Shirikisho la riadha nchini AK litafanya kikao mnamo jumatatu kufanya uamuzi wa uga utakaotumika kwa majaribio ya wanariadha watakaowakilisha kenya kwenye mashindano ya Olimpiki mwezi Julai. Rais wa shirikisho hilo Jackson Tuwei amesema wanariadha waliofuata taratibu za kukabiliana na ulaji muku ndio tu watakaoruhusiwa kushiriki majaribio. Tuwei alizungumza baada ya kuzuru uga wa Kipchoge Keino mjini Eldoret.