×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Raila asema kuwa kundi la BBI litakata rufaa kuhusu uamuzi wa mahakama kuharamisha mchakato wa BBI

15th May, 2021

Kwa mara ya kwanza kiongozi wa Odm Raila Odinga ambaye kwa pamoja waliasisi mchakato wa bbi na rais uhuru kenyatta amezungumzia uamuzi wa mahkama kuu ya kuharamisha bbi. Awali Raila alitaja mhimili wa mahakama kuwa asasi muhimu katika jukumu la usimamizi wa haki nchini. Raila ambaye alionekana kuwa mpole katika taarifa aliyotuma kwa vyombo vya habari amesema kuwa japo hajafurahishwa na maamuzi ya mahakama kuu kuhusu BBI, amewataka wakenya kuwa watulivu. Kadhalika amewahimiza wananchi kutolifanyia suala hilo kuwa la kibinafsi na kushambulia idara ya mahakama kwa uamuzi wake. Vivyo hivyo Raila amesema watatutumia njia ya kisheria kukabilia uamuzi huo kama vile kukata rufaa kwa sababu anaamini kuwa BBI inaungwa mkono na wengi. Kulingana naye utaratibu huu wa kutafuta ufasiri wa mahakama ya rufaa unatakiwa kufanywa kwa hekima na bila ubishi. Kwa mara nyingine amesisitiza kuwa juhudi za kuifanyia katiba marekebisho kupitia BBI zitaendelea kwa dhati ya moyo wake.  Amewakumbusha wakenya kuhusu safari ndefu ya kupigania demokrasia nchini mbali na mchakato wa katiba ya 2010. 

.
RELATED VIDEOS