12th May, 2021
Hatma ya Gavana wa Wajir Mohamed Mahmud, aliyetimuliwa na bunge la kaunti ya wajir sasa ipo kwenye bunge la seneti baada ya kamati ya maseneta 11 inayochunguza kutimuliwa kwake kuanza vikao leo. Bunge la kaunti ya Wajir kupitia wakili Ahmednasir Abdulahi, walikua wa kwanza kutoa ushahidi wake, ikitaka kamati hiyo kumwamrisha mkewe Gavana Mohamud na wanawe wawili kufika mbele ya kamati hiyo kutoa ushahidi kuhusu na kuhusika kwao kwenye madai ya ufisadi yaliyosabababisha kutimuliwa kwa gavana huyo. Hata hivyo kamati hiyo ilidinda kutoa amri hiyo. Gavana Mohamud atajitetea kesho mbele ya kamati hiyo.